Hifadhi ya picha ya Kibaha’i huruhusu kupakua picha zilizokusudiwa kwa madhumuni yasiyo ya kibiashara pekee.
Picha zinazohusiana na historia ya Imani Nchini, vilevile picha za waumini binafsi wenye umuhimu katika historia ya Imani Nchini
Picha za watu binafsi katika shughuli kama vile mikusanyiko ya Ibada, madarasa ya Watoto, vikundi vya vijana chipukizi na vikundi vya mafunzo, vile vile picha za wabaha’i pamoja na marafiki wa Imani wakichangia katika uboreshaji wa jamii.
Picha zinazohusiana na mkutano mkuu wa Kitaifa wa kila mwaka ambapo wawakilishi wa mkutano mkuu huchagua Baraza la Kiroho la Kitaifa kila baada ya Kipindi cha mwaka mmoja na hushauriana juu ya maendeleo ya Imani katika Nchi.