Kuhusu Imani

About Us

Imani ya Kibaháʼí Tanzania

Imani ya Kibaha'i ni dini ya Ulimwengu inayofundisha umoja wa Mungu, umoja wa dini, na umoja wa binadamu wote. Ilianzishwa na Mdhihirishaji wa Mungu kwa wakati huu Bahá'u'lláh mwaka 1844, ambaye alitambulisha ujumbe wa kiroho unaolenga kuunganisha wanadamu na kujenga dunia yenye haki, amani, na ustawi wa pamoja. Wabaha'i wanaamini kuwa Mungu ametuma Wadhihirishaji Wake katika nyakati mbalimbali—kama vile Ibrahimu, Musa, Krishna, Buddha, Yesu Kristo, Muhammad, na Bahá'u'lláh—ili kuwaongoza wanadamu katika safari yao ya kiroho na kuendeleza ustaarabu uendeleao. Imani ya Kibaha'i inasisitiza kanuni kama vile usawa wa wanawake na wanaume, elimu kwa wote, uondoaji wa ubaguzi wa rangi na dini, uadilifu wa kiuchumi, na uongozi wa haki unaotegemea mashauriano na huduma. Lengo lake kuu ni kujenga jamii inayodhihirisha upendo, umoja, na maendeleo endelevu ya kiroho na kimwili.

Imani ya Kibaha'i nchini Tanzania ilianza katika miaka ya 1950, na tangu wakati huo imeendelea kuenea kwa kasi katika mikoa mbalimbali ya nchi. Leo, Wabaha'i wa Tanzania wanashiriki katika juhudi za kijamii, kielimu, na kiroho zinazolenga kuboresha maisha ya watu wote bila ubaguzi. Shughuli kama Elimu ya kiroho ya watoto, Programu ya uwezeshaji kiroho wa vijana chipukizi, na Mikusanyiko kwaajili ya ibada ya pamoja na mashauriano ya jamii zinachochea moyo wa umoja na huduma. Wakiongozwa na kanuni za "Umoja katika Utofauti" na "Huduma kwa Binadamu," Wabaha'i nchini Tanzania wanaendelea kushirikiana na watu wa dini, tamaduni, na mataifa yote katika kujenga jamii yenye uadilifu, matumaini, na upendo—jamii inayodhihirisha maneno ya Bahá'u'lláh: "Dunia ni nchi moja, na binadamu ni raia wake."

Maendeleo ya Kiroho

Kuchangia katika mabadiliko ya jamii kupitia elimu ya kiroho na mikusanyiko kwaajili ya ibada ya pamoja.

Shughuli za Kijamii

Kupitia elimu na shughuli za kijamii, tunaimarisha jamii kote Tanzania.

Kujihusisha na Mijadala ya kijamii

Mijadala inayohusiana na uboreshaji wa jamii.

Maktaba

Pata na uangalie Maandiko Matakatifu, Vitabu, Barua, Miongozo, Nyimbo na nyenzo nyinginezo mtandaoni

Mikono wa Hoja ya Mungu
PDF Nyenzo za Kujiongezea Elimu
Maneno ya Mungu
PDF Sala
Idhini ya wazazi kwa ajili ya ndoa ya Kibahá’i
PDF Makusanyo
Nyenzo za Makongamano ya Kiulimwengu - Tanzania
PDF Nyenzo za Kujiongezea Elimu
Mfuko wa Kibahá’í
PDF Nyenzo za Kujiongezea Elimu
Nyumba ya Haki ya Ulimwengu
PDF Makusanyo
Maisha ya Ubikira na Matakatifu
PDF Makusanyo
Utakatifu wa Chaguzi za Kibahá’í
PDF Nyenzo za Kujiongezea Elimu

Blogu

Habari mpya, ujifunzaji, na tafakari za hivi karibuni kutoka kwa jumuiya yetu

MKUTANO WA USHAURIANO JUU YA FASIHI ZA KIBAHA'I Events
Oct 24, 2025 2120

MKUTANO WA USHAURIANO JUU YA FASIHI ZA KIBAHA'I

Mkutano wa mashauriano wenye hamasa na msukumo kuhusu kazi za fasihi za Kibahá’í ulifanyika 25-29 Septemba 2025 Bah...

Soma Zaidi
Umoja wa Binadamu Teachings
Oct 01, 2025 2018

Umoja wa Binadamu

Imani ya Baha'i inafundisha kwamba wanadamu ni familia moja na wakati umefika kwa muungano wake katika jamii moja ya kim...

Soma Zaidi

Wasiliana Nasi

Wasiliana nasi - tungependa kusikia kutoka kwako

Anwani

P.O.Box 585-Dar es Salaam

Simu

+255 685 637 422/+255 785 875 846

Barua Pepe

secretariat@bahai.or.tz