post-image

Kusudi la kimaadili lenye pande mbili

Vijana hutamani ukuaji wa kiroho, kiakili na kielimu na kutoa mchango wao kwenye ustawi wa binadamu.Wana uwezo mwingi mzuri, na kuuelekeza uwezo huo vizuri ni jambo muhimu, kwani ukielekezwa vibaya au ukitumika na wengine vibaya, inaweza kusababisha mateso mengi kwa jamii. Kushiriki katika programu za taasisi ya mafunzo kunawawezesha kujiona wenyewe kama wanaotembea katika njia ya huduma.

‘Abdu’l- Baha husema “ hakuna kitendo katika dunia ambacho ni cha kiungwana zaidi kuliko huduma kwa ajili ya manufaa kwa wote,” kwamba “uadilifu wa hali ya juu kabisa ni kuinuka na kwa bidii kujitoa wenyewe kwa huduma ya umma.” (‘Abdu’l-Baha, Siri ya Ustaarabu Mtakatifu; Wilmette: Baha’i Publishing Trust, 1990 aya. 130)

Katika huduma isiyo na ubinafsi kwa jamii kuna uwezekano wa yote mawili ukuaji binafsi na uzidishaji uwezo wa kuchangia kwenye maendeleo ya jamii. Kupitia kuelekeza vipaji na uwezo wao katika unyanyuaji hadhi ya jamii, ‘Abdu’l-Baha husema “wanakuwa sababu ya utulivu wa ulimwengu wa muumbo.” Kadri wanavyojaza shughuli zao za kila siku kwa moyo wa utoaji kwa ukarimu, na kufanya vitendo vya kujitolea kwa ustawi wa wengine, huvutia msaada na uthibitisho wa Mungu. (‘Abdu’l-Baha, Siri ya Ustaarabu Mtakatifu; Wilmette: Baha’i Publishing Trust, 1990 aya. 130)

Kiasili mambo mengi huchukua muda wa vijana, elimu, kazi, starehe, maisha ya kiroho, afya ya kimwili. Lakini wanajifunza kukwepa kuyaendea maisha kwa vipande vipande, mtazamo ambao hushindwa kuona uhusiano miongoni mwa sura mbalimbali za maisha.Mtazamo huo usio na mantiki mara nyingi humfanya mtu kuanguka na kuwa mwathiriwa wa uchaguzi bandia uliopendekezwa katika maswali kama vile mtu anapaswa kusoma au kutoa huduma, aendelee kimwili au achangie kwenye uboreshwaji wa wengine, ufuatiliaji wa masuala ya kazi au awe amejitoa wakfu kwa huduma. Kwa kupitia huduma, mtu anaweza kukuza maisha ambayo kwayo sura zake mbalimbali zinakamilishana. (Nyumba ya Haki ya Ulimwengu: Makongamano ya Vijana Julai – Oktoba 2013, Masomo kwa Washiriki; sehemu ya kwanza , Kipindi cha Ujana aya 3-5)

Mabadiliko haya ya pande mbili yatatokea tu kwa kupitia jitihada za makusudi, na ni muhimu kwamba vijana watambue maana yake kwa maisha yao na waweze kujawa na hisia thabiti ya malengo, kwa yote mawili, kuwajibika kwa ukuaji wao binafsi na kuchangia katika mabadiliko ya jamii. Wajibu pacha wa kimaadili kama huu utaonekana kwa kawaida kwenye maisha ya huduma.

Baha’u’llah husema “Jiwe la msingi la maisha ambayo hufuata njia ya Mungu ni ufuataji wa ubora wa kimaadili na upataji wa tabia iliyojawa na sifa ambazo hupendeza mbele ya macho Yake.” (Mkusanyo wa Dondoo kutoka Maandiko ya Kibaha’i, imekusanywa na Idara ya Utafiti ya Nyumba ya Haki ya Ulimwengu: London:Baha’i Publishing Trust, 1987)

Na pia huendelea kusema “ msijishughulishe na mambo yenu ninyi wenyewe; acheni mawazo yenu yakaziwe juu ya yale ambayo yatarekebisha bahati ya jamii ya binadamu na kutakasa mioyo na roho za watu.” (Makusanyo kutoka Maandiko ya Baha’u’llah, namba 43, uk. 105)

“Je, ni mahitaji gani? Upendo kwa wanadamu, unyoofu kwa wote, unaoakisi umoja wa ulimwengu wa ubinadamu, ufadhili, unaowashwa na moto wa upendo wa Mungu, ufikio wa maarifa ya Mungu na yale yanayofaa kwa ustawi wa mwanadamu.”

— ‘Abdu’l-Bahá